MADHARA YA DAWA MWILINI
Madhara ya Dawa Mwilini (Unwanted effects)(Kwa Uchache):
Dawa zinatusaidia sana kupambana na magonjwa na inabidi Zitumike kwa usahihi.
Zifuatazo ni baadhi tu ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa matumizi mabaya ya dawa kama ifuatazo:
1)Athari katika utendaji kazi wa moyo
•Dawa za High Blood Pressure ama BP kama ilivyozoeleka, huweza kuathiri utendaji kazi wa moyo na kusababisha Hypotension (Presha ya kushuka) Zipo dawa zingine pia zinazoweza kuleta athari .
2)kuvuja damu kusikozuilika (Hemorragic effect)
•Dawa ambazo hutumika kuzuia kuganda kwa damu mfano mzuri (Heparine na Asprine) huweza kusababisha kuvuja kwa damu ndani au nje ya mwili, mfano mgonjwa wa vidonda vya tumbo yuko katika hatari ya kupata athari hii iwapo atatumia dawa hizo.
3)Athari kazi kwenye Figo na Ini.
•Figo na Ini ni moja kati ya Viungo muhimu mwilini husaidia katika kuvunja vunja dawa na kuzitoa mwilini baada ya kutumiwa na mwili, Dawa nyingi huleta athari kwenye viungo hivi haswa zinaponywewa kwa kiwango kikubwa, mfano mzuri ni PARACETAMOL, itakapotumiwa katika dozi inayozidi 4g/day basi Ini huweza kushindwa kufanya kazi na kuleta madhara makubwa kiafya
4)Kushuka kwa Sukari mwilini (Hypoglycemia)
•Kushuka kwa kiwango cha sukari mwilini ni hatari sababu athari hii inaweza sababisha kifo cha ghafla (Sudden Death) Dawa kama TRAMADOL inayotumika sana Kwenye maumivu makali huweza kuwa moja wapo ya dawa zinazoweza sababisha athari hii. (Zipo nyingine nyingi)
5)Kupanda kwa kiwango cha potassium mwilini (Hyperkaliemia)
•Potassium husaidia sana kazi nyingi mwilini ikiwamo utendaji kazi wa moyo, kiwango hichi kinapopanda ghafla huweza kuleta athari haswa katika utendaji kazi wa moyo. Dawa kama IBUPROFEN (NSAID), AMILORIDE na zingine nyingi huweza kuleta madhara haya (zipo nyingine nyingi).
Usinywe Dawa Kiholela bila ushauri wa Wataalam, Maliza dozi yote kwa wakati.
usisahau kutuandikia kwa msaada zaidi 🤟🏽
Comments
Post a Comment